Raphina kukabidhi maisha yake ya soka Barcelona


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

“Ndiyo, nina mpango wa kuongeza mkataba na nitafurahi sana kuweza kuongeza mkataba wangu na kwa matumaini kumaliza maisha yangu ya soka Barcelona,” amesema Raphinha, akieleza nia yake ya kuendelea kuichezea Barcelona kwa kipindi chake chote akiwa kama mchezaji.

Kauli hiyo ya Raphinha imekuja wakati ambapo mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa mshambuliaji huyo na Barcelona yanaendelea.

Raphinha, ambaye amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Barcelona, ameweka wazi kuwa anataka kuendelea kubaki katika klabu hiyo badala ya kuanza sura mpya katika klabu nyingine.

Mchezaji huyo ameeleza kuwa lengo lake ni kufikia makubaliano yatakayomuwezesha kuongeza muda wake wa kuitumikia Barcelona na hatimaye kumalizia maisha yake ya soka akiwa na klabu hiyo.

Kauli hiyo pia inaonyesha namna Raphinha anavyoiona Barcelona kama sehemu ya mwisho ya safari yake ya soka, huku mazungumzo ya mkataba mpya yakiendelea kati ya pande hizo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments