Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Msimu wa 2026/27 umeanza, lakini Kwa Paris Saint-Germain (PSG) tayari wanakutana na matokeo yanayowapa maswali ya kujiuliza.
Baada ya kucheza michezo mitatu, PSG hawajapata ushindi, wakitoka sare katika michezo miwili na kupoteza mmoja, Matokeo hayo yamewaacha wakiwa na alama mbili katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi one.
Hali hiyo inakuja baada ya msimu uliopita ambao PSG walifanya vizuri katika mashindano ya ndani na Ulaya, wakitawala Ligue 1 na kutwaa UEFA Champions League.
Katika soka, mafanikio ya muda mrefu mara nyingi hufuatiwa na kipindi ambacho timu inahitaji kujipanga upya hapo Wachezaji, mfumo wa uchezaji na mipango ya benchi la ufundi huweza kuhitaji mabadiliko ili timu iendelee kuwa na ushindani.
Hata hivyo, bado ni mapema kusema PSG wameingia kwenye kipindi cha anguko wakati ambao ndio kwanza Msimu umeanza na michezo michache iliyochezwa haiwezi kutoa picha kamili ya uwezo wa timu kwa msimu mzima.
Kinachobaki ni PSG kutumia kipindi hiki kurekebisha mapungufu na kurejesha matokeo endapo hali itaendelea hadi msimu ukawa mgumu, hapo ndipo mjadala wa kujenga kizazi kipya unaweza kuanza, hasa baada ya mafanikio waliyoyapata msimu uliopita.
Kwa sasa, PSG wanahitaji zaidi majibu uwanjani kuliko hukumu kuhusu mustakabali wa timu.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment