Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kocha wa zamani wa Manchester City, Pep Guardiola, ametuma ujumbe kwa mashabiki na Wadau wa klabu hiyo kupitia njia ya mtandao, akisisitiza kuwa yupo pamoja nao licha ya kuondoka kwenye nafasi ya ukocha.
Guardiola, ambaye alikabidhi mikoba kwa Enzo Maresca mwishoni mwa msimu uliopita, amesema ataendelea kuisapoti City pamoja na uongozi, wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki.
“Nataka kila shabiki wa Manchester City ajue kwamba nipo hapa, zaidi kuliko wakati mwingine wowote,” amesema Guardiola.
Ujumbe huo umefika baada ya City kukabiliwa na tuhuma za ukiukaji wa kanuni za kifedha, huku klabu hiyo ikiwa imeeleza kuwa itakata rufaa.
Guardiola aliongoza City kwa miaka 10 kabla ya kuondoka mwaka 2026, akitwaa Jumla ya mataji 20 akiwa klabuni hapo.
Hii inataia faraja kwa klabu kuwa watu wake wa karibu licha ya kuwa nje ya klabu bado umoja na mshikamano unaendelea kuonekana.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment