Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa Tanzania, Clara Luvanga, ameandika sura mpya katika soka la wanawake Duniani baada ya uhamisho wake kuelekea Washington Spirit ya Marekani akitokea Al Nassr ya Saudi Arabia.
Uhamisho huo umegharimu dola milioni 2.3, sawa na takribani Billion 6 za kitanzania na kumweka nyota huyo kileleni mwa orodha ya wachezaji waliohamishwa kwa ada kubwa katika historia ya soka la wanawake.
Kabla ya Luvanga, rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Felicia Schroder baada ya kuondoka BK Hacken ya Sweden na kujiunga na Real Madrid kwa ada ya zaidi ya dola milioni 1.6.
Schroder anafuatiwa na Kerolin, ambaye alihama Manchester City kwenda Barcelona kwa dola milioni 1.6, kabla ya Lizbeth Ovalle kushika nafasi ya nne baada ya kuhamia Orlando Pride akitokea Tigres kwa dola milioni 1.5.
Nafasi ya tano inakamilishwa na Olivia Smith, aliyesajiliwa na Arsenal kutoka Liverpool kwa dola milioni 1.36.
Kwa maana hiyo, Luvanga si tu amebadilisha klabu, bali pia ameweka Tanzania kwenye orodha ya mataifa yaliyowahi kutoa mchezaji aliyehusika katika uhamisho wenye gharama kubwa zaidi kwenye soka la wanawake duniani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment