Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Historia ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa ukanda wa Afrika Mashariki imekuwa na majina machache, huku Ethiopia na Sudan zikiwa miongoni mwa mataifa yaliyowahi kufika kileleni mwa mashindano kwa kutwaa taji hilo.
Ethiopia ilitwaa ubingwa mwaka 1962, kabla ya Sudan kufanya hivyo mwaka 1970, na tangu wakati huo hakuna taifa jingine kutoka ukanda wa Afrika Mashariki lililofanikiwa kuongeza jina lake kwenye orodha ya mabingwa.
Hivyo, kuelekea AFCON 2027, ambapo Tanzania, Kenya na Uganda zitakuwa wenyeji kwa pamoja, macho yanaelekezwa zaidi kwenye mataifa hayo matatu kuona kama yataweza kutumia nafasi ya kucheza mbele ya mashabiki wao kuvunja mwiko uliodumu kwa nusu Karne.
Kwa Tanzania, Kenya na Uganda, mashindano hayo yatakuwa nafasi ya kuonyesha maendeleo ya soka la Afrika Mashariki, lakini pia yatatoa fursa ya moja ya mataifa hayo kupigania nafasi ya kuwa bingwa wa kwanza wa ukanda huo baada ya miaka 56.
Uwanja wa nyumbani unaweza kuwa sehemu ya msukumo kwa wenyeji kutokana na kuungwa mkono na mashabiki, lakini hilo pekee halitoshi bila maandalizi, kikosi chenye ushindani na uwezo wa kushinda michezo dhidi ya mataifa yenye uzoefu katika mashindano hayo.
AFCON 2027 inaweza kuwa zaidi ya mashindano kwa Afrika Mashariki, kwani Tanzania, Kenya na Uganda zitakuwa na nafasi ya kujaribu kuvunja historia iliyodumu kwa zaidi ya nusu karne.
Swali linalobaki ni je , baada ya Ethiopia na Sudan, ni taifa gani la Afrika Mashariki litakalofuata kutwaa AFCON?
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment