Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Real Madrid, Kylian Mbappe, amesema kama angepewa nafasi ya kupiga kura katika tuzo ya Ballon d’Or, angejichagua mwenyewe kushinda tuzo hiyo.
Nyota huyo ametoa kauli hiyo akieleza kuwa Ballon d’Or ni tuzo ya mchezaji binafsi, hivyo kinachopaswa kuangaliwa ni kile ambacho mchezaji amefanya katika kiwango chake binafsi, badala ya kuangalia mataji aliyoshinda akiwa na timu.
Kauli hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa mjadala kuhusu nafasi yake katika mbio za tuzo hiyo, huku baadhi wakitaja kutokuwepo kwa mafanikio ya timu kama hoja dhidi yake.
Hata hivyo, amesema hajawahi kuona mshindi wa Ballon d’Or aliyekidhi kila kigezo kinachotumika kumpata mshindi wa tuzo hiyo.
“Ni tuzo ya mtu binafsi, tunahitaji kuangalia kile ambacho mchezaji alifanya binafsi, watu wanasema sikuwa na taji, lakini sijawahi kuona mshindi wa Ballon d’Or aliyekidhi kila kigezo,” alisema Mbappe.
Mshambuliaji huyo pia ametaja rekodi yake ya kuwa mfungaji bora katika historia ya Kombe la Dunia kama moja ya mambo yanayopaswa kuzingatiwa katika mjadala huo.
Mbappe ameendelea kusisitiza kuwa kuwa mfungaji bora katika mashindano makubwa ambayo hukutanisha wachezaji wa kiwango cha juu, ikiwemo Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia, ni sehemu ya mafanikio yake binafsi.
Kwa kuangalia alichofanya yeye na kile kilichofanywa na wachezaji wengine katika msimu huo, amesema haoni kama angekuwa amemnyang’anya mtu tuzo endapo angeishinda.
Pamoja na msimamo huo, Mbappé amesema anaelewa kuwa wapo watu ambao hawatakubaliana naye, akisisitiza kuwa kila mpiga kura ana mtazamo wake kuhusu Ballon d’Or.
“Naelewa watu wanaopinga. Hii siyo udikteta na kila mtu ana maoni yake kuhusu Ballon d’Or,”
TAKWIMU ZINAZO MBEBA MBAPPE KUELEKEA BALLON D'OR
Mfungaji bora wa muda wote kombe la Dunia 22.
Mfungaji bora wa UEFA champions league 15.
Mfungaji Bora wa Laliga 25.
Takwimu za msimu wa 2025/26.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment