Mstari unaopotea uwanjani na kazi yake katika mpira wa miguu



Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.


Katika soka, wakati mwamuzi anapotoa mpira wa adhabu, moja ya majukumu yake ni kuhakikisha wachezaji wa timu inayolinda wanaheshimu umbali unaotakiwa kutoka kwenye mpira.

Kwa mujibu wa sheria, ukuta unatakiwa kuwa umbali wa angalau mita 9.15 kutoka kwenye mpira, Changamoto ilikuwa namna ya kuhakikisha wachezaji hawasogei mbele na kupunguza umbali huo wakati mwamuzi akiwa anasimamia maandalizi ya mpira huo.

Hapo ndipo ilipoingia vanishing spray, inayotumiwa na mwamuzi kuchora mstari kwenye uwanja. Mstari huo huonyesha eneo ambalo ukuta unatakiwa kusimama, huku mpira ukiwekwa upande mwingine wa alama hiyo.


Wazo la kutumia dawa hiyo lilianza kujadiliwa rasmi na IFAB ( International Football Association Board) mwaka 2010, kabla ya majaribio kuidhinishwa mwaka 2011 baada ya kuonekana inaweza kusaidia waamuzi katika kusimamia umbali wa ukuta.

Kutokana na majaribio hayo, matumizi yake yakaendelea kuenea katika mashindano mbalimbali na kufikia hatua ya kutumika kwenye Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2014 nchini Brazil.

Jambo muhimu ni kwamba vanishing spray haikubadilisha sheria ya mita 9.15. Badala yake, ilileta njia rahisi ya kumsaidia mwamuzi kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa wakati wa mpira wa adhabu.


Baada ya muda mfupi, mstari huo hutoweka wenyewe, hivyo, alama hiyo huwa ya muda na haiathiri uwanja baada ya mchezo kuendelea.

Kwa mtazamo huo, vanishing spray ni mfano wa namna vifaa rahisi vinavyoweza kutumika kusaidia mwamuzi katika kutekeleza sheria za mchezo bila kubadilisha msingi wa sheria yenyewe.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments