Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani miezi sita kutokana na majeraha mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize, amerejea dimbani katika mchezo dhidi ya Geita Gold, akifungua tena ukurasa wa safari yake ndani ya uwanja baada ya kuingia akitokea benchi akichukua nafasi ya Selemani Mwalimu.
Urejeo huo umekuja wakati ambao mashindano ya AFCON yanazidi kukaribia, hivyo kurudi kwake kwenye ushindani ni habari njema kwa Yanga na Taifa Stars huku kwa upande wa Yanga kukizidi kuongeza upana wa kikosi chao.
Mzize ni miongoni mwa washambuliaji wanaotegemewa na Taifa Stars, hiyo, kupata nafasi ya kurejea kucheza katika kipindi hiki kunampa nafasi ya kurejesha utimamu wa ushindani na kuendelea kujenga kiwango chake kupitia michezo ya klabu.
Kwa Yanga, kurejea kwake kunaongeza chaguo katika safu ya ushambuliaji baada ya mashabiki kusubiri kwa muda kumuona tena mshambuliaji huyo akirudi kwenye majukumu yake.
Zaidi ya hapo, urejeo wa Mzize una maana kwa Taifa Stars wakati ambao AFCON inakaribia, kila mchezaji anayehitajika kwenye kikosi cha taifa anapokuwa fiti na akipata dakika za mchezo, huongeza chaguo kwenye benchi la ufundi.
Hivyo, Mzize kurejea si habari njema kwa Yanga pekee, bali pia kwa Taifa Stars ambayo inahitaji washambuliaji hasa baada ya Samatta kutundika daruga akiwa kama mshambuliaji. kwa sasa Tanzania inahitaji mshambuliaji kama mzizie akiwa kwenye ubora wake huku michezo ya kimataifa kwa upande wa klabu ikitarajia kuongeza ubora wake kuelekea Afcon.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment