Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji raia wa Argentina Lionel Messi
ameendelea kufukuzia na kuvunja rekodi katika soka, baada ya kufikisha mabao 76
ya mipira ya adhabu (free-kick), akibakiza mabao mawili kuwa kinara wa muda
wote.
Messi sasa anashika nafasi ya pili kwenye
orodha ya wafungaji bora wa free-kick akiwa na mabao 76, nyuma ya Mbrazil
Marcelinho Carioca anayeshikilia rekodi hiyo kwa mabao 78.
Katika orodha hiyo, Jair Rosa Pinto
anashika nafasi ya tatu akiwa na mabao 74, akifuatiwa na Roberto Dinamite
mwenye 73 huku Juninho Pernambucano akiwa na 72.
Kwa kufikisha mabao hayo, Messi ameendelea
kusogea karibu na kuvunja rekodi iliyodumu kwa muda mrefu, huku akihitaji mabao
mawili pekee kumpita Carioca na kuwa kinara wa muda wote wa ufungaji wa
free-kick.
Hatua hiyo inaongeza rekodi nyingine kwenye
historia ya Messi, ambaye katika kipindi hiki cha mwisho cha maisha yake ya
soka bado anaendelea kuweka alama katika takwimu mbalimbali.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment