Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Derby ya Manchester imeendelea kuandika historia yake baada ya Manchester City kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa Old Trafford.
Bao hilo lilifungwa na Erling Haaland, ambaye kwa kufunga kwake ameweka jina lake kwenye historia ya Derby ya Manchester, akifikisha mabao tisa katika michezo minane dhidi ya United kwenye Premier League.
Haaland sasa amekuwa mfungaji mwenye mabao mengi zaidi katika Derby ya Manchester kwenye historia ya Premier League, akiwapita Sergio Aguero na Wayne Rooney ambao kila mmoja ana mabao nane.
Aguero alifanya hivyo kwenye michezo 13 kufikisha mabao hayo, wakati Rooney alifanya hivyo katika michezo 21. Haaland, kwa upande wake, amefikisha mabao tisa katika michezo minane pekee nakujitwalia utawala wa ufungaji kwenye Derby hiyo.
Rekodi hiyo inaonyesha namna mshambuliaji huyo wa Manchester City alivyojenga historia katika mchezo huu wa jadi wa jiji la Manchester. Kila anapokutana na United, Haaland amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaotazamiwa kubeba jukumu la kuamua matokeo.
Ushindi wa City wa bao 1-0 Old Trafford umeongeza sura nyingine kwenye historia ya Derby ya Manchester, huku Haaland akiendelea kuacha rekodi yake katika mchezo huo. Kinacho subiriwa ni Kuona kama Kuna mchezaji ataivunja historia hiyo au Halaand ataendelea kuliandika jina lake kama sehemu ya historia ya mchezo huo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment