Kisa heshima Simba na Yanga Zapumuliana Kisogoni


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Michezo mitano ya kwanza ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara imezifanya Simba na Yanga kuanza mbio za ubingwa kwa kasi, huku kila timu ikiwa imekusanya alama zote 15 pasipo kudodosha alama yoyote .

Hali hiyo si mpya kwa timu hizo na inatokea mara chache kwa baadhi ya misimu, kwa zaidi ya misimu kumi iliyopita, Simba na Yanga zimewahi kufikisha alama 15 baada ya michezo mitano katika misimu ya 2019/20 na 2024/25 huku msimu wa 2026/27 ukiongezeka kwenye orodha hiyo.

Msimu huu, timu hizo zimeonekana kupambana kwa nguvu zao kuhakikisha kuwa zinatwaa ubingwa , hiyo inachagizwa na ushindani wa klabu hizo katika historia zao za hivi karibuni. Yanga anahitaji kuongeza idadi ya ubingwa kwa kuchukua mara ya sita mfululizo huku mnyama akihitaji kuvunja uteja mbele ya watani wao, vita hiyo inafanya vilabu hivyo kupambana kuhakikisha haviangushi alama kirahisi kwaajili ya kujitengenezea heshima kwa Kila mmoja.


Kwa kuwa misimu ya hivi karibuni imeonyesha ubingwa huamuliwa kwa tofauti ndogo ya alama, kila mchezo unakuwa na umuhimu katika safari ya kuwania taji.

Iwapo Simba na Yanga zitaendelea kukusanya alama kwa kasi hii, mbio za ubingwa zinaweza kuamuliwa katika michezo ya mwisho ya msimu huku michezo baina Yao inatarajiwa kuongeza taswira ya bingwa wa msimu huu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments