Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA, Gianni Infantino, ametangaza kugombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwaka 2027, licha ya kukabiliwa na upinzani kutoka baadhi ya viongozi wa soka barani Ulaya.
Hatua hiyo inakuja baada ya Infantino kukumbana na tuhuma na ukosoaji kuhusu uongozi wake kufuatia baadhi ya matukio yaliyotikea wakati wa Kombe la Dunia, pamoja na sakata la mpango wa kuuza hisa.
Pamoja na changamoto hizo, Infantino amesema yuko tayari kuendelea kuongoza FIFA, huku uchaguzi huo ukitarajiwa kufanyika Machi 2027.
Kwa upande mwingine, upinzani kutoka UEFA unatajwa kuwa moja ya changamoto atakazokutana nazo katika harakati za kutafuta muhula mwingine.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment