Haaland aendelea kuitikisa orodha ya wafungaji bora muda wote UEFA nations League


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Norway, Erling Haaland, anaendelea kutawala orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa UEFA Nations League, akionyesha uwezo wake wa kuzifumania nyavu katika michuano hiyo.

Haaland amefikisha mabao 21 katika michezo16, akimzidi Aleksandar Mitrovic wa Serbia na Cristiano Ronaldo wa Portugal ambao kila mmoja ana mabao 15, nyota huyo amefikia idadi hiyo ya mabao baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Dermark kwenye ushindi wa 3-2.

Uwezo wa Haaland wa kutumia nafasi, nguvu zake ndani ya eneo la hatari na uwezo wa kumalizia mipira umemfanya kuwa mmoja wa washambuliaji wanaotajwa zaidi katika kizazi cha sasa.


Orodha ya wafungaji bora wa muda wote Nations League

1. Erling Haaland – Norway: 21

2. Aleksandar Mitrovic – Serbia: 15

3. Cristiano Ronaldo – Portugal: 15

4. Vedat Muriqi – Kosovo: 14

5. Romelu Lukaku – Belgium: 13

6. Viktor Gyokeres – Sweden: 10

7. Edin Dzeko – Bosnia and Herzegovina: 9

8. Christian Eriksen – Denmark: 9

9. Kylian Mbappe – France: 9

10. Danel Sinani – Luxembourg: 9

Orodha hiyo inaonyesha namna Haaland alivyoweka pengo dhidi ya washambuliaji wengine, huku Ronaldo na Mitrovic wakiwa mabao sita nyuma yake kwa upande wa mabao.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.




0/Post a Comment/Comments