Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imeipa Simba SC muda zaidi wa kujiandaa na mchezo wa klabu bingwa Afrika kabla ya mchezo wake dhidi ya Azam FC baada ya mchezo huo kusogezwa mbele hadi Septemba 16, 2026, badala ya Septemba 9.
Simba iliwasilisha ombi kwa Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) la kusogezwa kwa mchezo huo ili kupata nafasi ya kujiandaa na mchezo wa marudiano wa CAF Champions League dhidi ya Mighty Wanderers.
Kwa ratiba mpya, Simba itaanza hatua hiyo kwa kucheza na Mighty Wanderers Septemba 6, kabla ya kukutana tena na timu hiyo Septemba 13, kisha kucheza dhidi ya Azam FC Septemba 16.
Mabadiliko hayo yanaipa Simba muda wa kutosha katika michezo yake, jambo linaloweza kuisaidia benchi la ufundi kufanya tathmini ya mchezo wa kwanza dhidi ya Mighty Wanderers na kusahihisha maeneo yatakayohitaji maboresho kabla ya mchezo wa marudiano.
Aidha, muda huo utapunguza changamoto ya kuharibika kwa mipango ya mwalimu kutokana na majeraha ambayo huenda wachezaji wangeweza kuyapata katika mchezo dhidi ya Azam FC ikiwa ungechezwa Septemba 9.
Kwa upande mwingine, wachezaji wa Simba watapata muda wa kutosha wa kupumzika kabla ya mchezo wa marudiano na kuwafanya wawe timamu kwa asilimia kubwa kwenye mchezo wa marudiano.
Pia kusogezwa mbele kwa mchezo huo kutaufanya uwe wa ushindani na kuvutia kuliko mchezo ungechezwa Septemba 9. Simba wangecheza kwa tahadhari wakiwaza mchezo wa marudiano.
Ikumbukwe Simba na Azam ni miongoni mwa michezo mikubwa katika ligi na unatazamwa zaidi hivyo kuupeleka mbele kunato fursa kwa timu hizo kuwa na mchezo mzuri wenye ushindani pindi watakapo kutana.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment