Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mchezo wa MLS kati ya Chicago Fire na Inter
Miami uliomalizika kwa sare ya 1-1, lakini kilichozungumzwa zaidi baada ya
mchezo huo ni maneno ya Rodrigo De Paul kwa Robert Lewandowski.
Katika dakika za mwisho kulitokea
purukushani miongoni mwa wachezaji huku lewandowski akihusika , katika mzozo
huo De Paul alimtaka Lewandowski ajieleze kuhusu mafanikio yake akiwa mchezaji
wa timu ya taifa,huku akitaja kuwa yeye
ameshinda Copa America mbili pamoja na Kombe la Dunia.
"WEWE NI NANI? MIMI NIMEBEBA COPA
AMERICA MBILI NA KOMBE LA DUNIA, WEWE UMEBEBA NINI?" Swali la DePaul kwa
lewandowski.
Kauli hiyo ilimrudisha Lewandowski kwenye
mjadala ambao umekuwepo kwa miaka kadhaa; je, mchezaji hupimwa zaidi kwa
mafanikio ya klabu au kwa kile alichofanya kwenye timu ya taifa?
Lewandowski ana historia iliyojengwa
kupitia mabao, akiwa Bayern Munich, aliisaidia timu hiyo kushinda mataji
mbalimbali, ikiwamo Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2019/20. Baadaye alihamia
Barcelona na kuendelea kuwa sehemu ya timu iliyopambana kwa ajili ya mataji
nchini Hispania.
Hata hivyo, tofauti yake na De Paul
inaonekana zaidi wanapozungumzia timu za taifa, De Paul alikuwa sehemu ya
Argentina iliyoshinda Copa America na baadaye Kombe la Dunia, Mafanikio hayo
yameipa Argentina historia ambayo Poland haijapata katika kipindi ambacho
Lewandowski amekuwa kinara wa timu hiyo.
Ndiyo maana maneno ya De Paul yanaweza
kumuumiza Lewandowski katika mjadala wa mafanikio ya kimataifa, lakini hayawezi
kufuta kile ambacho mshambuliaji huyo amefanya katika ngazi ya klabu.
Kwa hiyo, tatizo si kwamba Lewandowski
hajafanya kitu, tatizo ni kwamba katika soka la kimataifa, historia yake
haijafikia kilele ambacho De Paul tayari amekifikia.
Hapo ndipo tofauti yao ilipo, Lewandowski
ana mabao na mataji ya klabu, wakati De Paul ana historia ya kushinda mataji
makubwa akiwa na Argentina.
Na katika mchezo ambao kila kizazi hutafuta
alama ya kuacha, hilo ndilo lililofanya kauli ya De Paul kuhusu Lewandowski
kuibua mjadala mkubwa baada ya sare hiyo ya MLS.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment