TFF yatangaza kufungwa kwa dirisha la usajili kwa vilabu Tanzania



Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Dirisha la usajili kwa klabu zinazoshiriki mashindano ya soka nchini linafungwa leo, Agosti 15, 2026, huku baadhi ya timu zikikamilisha usajili wao wa mwisho kuelekea msimu wa 2026/2027.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), dirisha hilo litafungwa saa 5:59 usiku na hakutakuwa na muda wa nyongeza.

Dirisha hilo linawahusu klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC, NBC Championship, First League, Ligi Kuu ya Vijana NBC U20 na Ligi Kuu ya Wanawake.

Hadi kufikia leo, baadhi ya klabu bado hazijafanya usajili wa mchezaji hata mmoja kupitia mfumo wa FIFA Connect. Klabu hizo ni Kengold FC inayoshiriki Championship na Mount Hanang ya First League.

Kwa upande mwingine, klabu nyingine zimekuwa zikikamilisha usajili wa wachezaji katika siku za mwisho za dirisha hilo, hatua inayozifanya ziingie katika msimu mpya zikiwa zimekamilisha sehemu kubwa ya mipango ya vikosi vyao.

Baada ya muda wa usajili kufungwa, klabu hazitapewa muda wa ziada kuwasilisha usajili kupitia dirisha hilo.

Hatua hiyo inatarajiwa kuhitimisha shughuli za usajili wa msimu wa 2026/2027, huku klabu zikielekeza nguvu katika mashindano taliyopo mbele Yao.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments