Wanaume watatu tishio nafasi nne za juu NBC premier league


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Msimamo wa nne bora katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2026/27 unaweza kubadilika msimu huu, baada ya Mbeya City, Geita Gold na Polisi Tanzania kuanza kuonyesha ushindani katika mbio za nafasi za juu.

Kwa misimu ya hivi karibuni, nafasi ya pili na ya tatu zimekuwa zikishikiliwa na Azam FC pamoja na Singida Black Stars hata hivyo, mwanzo wa msimu huu umeonyesha kuwa timu hizo zinaweza kukutana na ushindani kutoka kwa timu nyingine.

Baada ya michezo minne kwa timu hizo, Mbeya City inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama tisa ikipata ushindi katika michezo mitatu na kupoteza mmoja kwa Geita Gold yenyewe inashika nafasi ya tano ikiwa na alama saba, ikiwa nyuma ya Azam FC wenye alama nane huku Singida Black stars ikiwa na alama Saba nafasi ya sita, huku Polisi Tanzania ikiwa nafasi ya saba alama Saba.

Msimamo huo unaonyesha kuwa tofauti ya alama kati ya timu zinazowania nafasi za juu bado ni ndogo hivyo, matokeo ya michezo inayofuata yanaweza kubadilisha mpangilio wa msimamo kwa timu hizo.

Mbeya City, Geita Gold na Polisi Tanzania zikiendelea na kiwango chao na kupata matokeo katika michezo inayofuata, zinaweza kuingia katika ushindani wa moja kwa moja wa nafasi ya pili na tatu.

Kwa upande mwingine, Azam FC na Singida Black Stars zitahitaji kuendelea kupata matokeo ili kulinda nafasi zao na kuzuia timu hizo kuwapita katika mbio za nne bora.

Mwisho wa msimu, nafasi hizo zina umuhimu kutokana na nafasi ya timu zinazomaliza juu katika msimamo kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa, kwa kuzingatia nafasi zinazotolewa kwa Tanzania.

Kwa hiyo, kama ushindani huu utaendelea, mbio za nafasi nne za juu msimu huu zinaweza kuwa tofauti na ilivyozoeleka katika misimu ya nyuma, huku nafasi ya pili na ya tatu zikiwa miongoni mwa maeneo yanayoweza kubadilika.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments