X-Factor wa Yanga wazo jipya kurudisha pesa ya usajili kwa wachezaji wakubwa Tanzania

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Utambulisho wa mchezaji mpya umechukua sura nyingine katika soka la Tanzania baada ya Yanga kuandaa tukio maalumu la kumtambulisha Stephan Aziz Ki katika Uwanja wa KMC Complex siku ya agosti 15, 2026.

Aziz Ki, ambaye kwa muda alikuwa akizungumziwa chini ya jina la siri “X Factor”, hatimaye ameonyeshwa mbele ya mashabiki katika tukio lililochanganya utambulisho wa mchezaji na burudani huku kabla ya utambulisho wake, mara kadhaa alionekana akifanya mazoezi ya pamoja na timu na kwa nyakati tofauti tofauti ameonekana akiwa pamoja na viongozi wa timu wakati ambao ulisubiriwa ufike, usajili ukamilike na hatimaye ni mwananchi.

Mfumo huu si mgeni katika soka la dunia ambapo vilabu vikubwa vimekuwa vikitumia utambulisho wa wachezaji wakubwa kama matukio ya kuwavuta mashabiki na kuongeza mapato kupitia utambulisho wa mchezaji pekee pasipo kuhusishwa na mchezo. Real Madrid ilifanya hivyo ilipomtambulisha Kylian Mbappe katika Uwanja wa Santiago Bernabeu mbele ya mashabiki wengi na Trabzonspor ya Uturuki wamefanya hivyo wakimtambulisha Mohamed Salah hivi karibuni.

Kwa sasa Yanga imeleta mtindo huo katika mazingira ya Tanzania ambapo tofauti ni kwamba klabu haikufanya utambulisho wa Aziz Ki kama sehemu ya utambulisho wa kawaida wa wachezaji, bali iliandaa tukio maalumu.


Uamuzi huo ulifuatia kutotambulishwa kwa Aziz Ki katika tamasha la Yanga Day iliyofanyika Agosti 9, 2026, Badala ya kukosa nafasi katika utambulisho wa pamoja hivyo klabu imetengeneza tukio maalumu, hatua iliyompa nafasi ya kutambulishwa tofauti.

Kwa upande wa klabu, tukio hilo limekuwa na faida ya kibiashara ambapo Yanga imepata nafasi ya kukusanya mapato kutokana na mahudhurio ya mashabiki kwenye tukio hilo, fedha ambazo zinaweza kusaidia mipango mingine ya klabu na kurudishia kiasi fulani kilichotumika kwenye usajili.

Hii inaonyesha namna usajili wa mchezaji unavyoweza kutumika kama sehemu ya kuongeza mapato, Mchezaji mwenye mvuto au ufuasi mkubwa anaweza kuwa sababu ya mashabiki kuhudhuria tukio, kununua bidhaa za klabu na kushiriki katika shughuli zinazohusiana na utambulisho wake.

Jambo lingine lililofanya tukio hilo kuwa tofauti ni muda wake, kwa siku moja Yanga imekuwa na mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo katika uwanja wa majaliwa Stadium Lindi, wakati utambulisho wa Aziz Ki ukiendelea KMC Complex ambapo pia mashabiki walipata fursa ya kuangalia mchezo kwenye big screen.


Tukio hilo linatoa funzo kwa vilabu nchini kuwa vinaweza kutumia fedha nyingi katika usajili wa mchezaji mkubwa na pia vinaweza kurudishia pesa kiasi au yote kupitia kumtambulisha mchezaji mmoja kwa kutengeneza tamasha la kipekee lkama walivyo Fanya yanga.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments