Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Vinicius Jr, ameanza mazoezi na kikosi hicho kuelekea michezo ya maandalizi ya msimu mpya, baada ya siku kadhaa za taarifa zinazomhusisha na uwezekano wa kujiunga na Arsenal.
Tetesi hizo zilianza kusambaa kufuatia kutokamilika kwa mazungumzo ya kuongeza mkataba wake na Real Madrid, hali iliyozua taarifa kwamba Arsenal ilikuwa ikifuatilia maendeleo ya mchezaji huyo.
Hata hivyo, Vinicius amerejea kwenye mazoezi na Real Madrid pamoja na wachezaji wengine waliohitimisha mapumziko yao, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu wa 2026/27.
Kurejea kwake kunamaanisha anaendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Real Madrid wakati klabu hiyo ikiendelea na maandalizi yake, huku suala la mkataba mpya likisubiri hatua za mazungumzo kati ya pande husika.
Vinicius, ambaye ameichezea Real Madrid kwa misimu kadhaa, bado ana mkataba unaoendelea na klabu hiyo, wakati mustakabali wake ukiendelea kufuatiliwa katika dirisha hili la usajili.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment