Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Tangu Lionel Messi ajiunge na Inter Miami mwaka 2023, ameendelea kuweka rekodi ya ushiriki wake katika michezo ya klabu hiyo kwa kuwa na mchango mzuri katika upajikaji na utoaji pasi za mwisho za mabao.
Katika kipindi hicho, Messi amecheza jumla ya michezo 111, akifunga mabao 98 na kutoa pasi za mabao 53.
Kwa takwimu hizo, mshambuliaji huyo wa Argentina amehusika moja kwa moja katika mabao 151 ya Inter Miami, akihusishwa na mabao kupitia ufungaji na utoaji wa pasi za mwisho.
Aidha, rekodi hiyo inaonyesha mchango wake tangu alipowasili katika klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS).
Messi anaendelea na safari yake ya soka akiwa katika hatua ambayo rekodi hizo zinaweza kuendelea kubadilika kutokana na idadi ya michezo atakayocheza na mabao atakayofunga.
Kwa sasa, takwimu zake Inter Miami zinaonyesha: michezo 111, mabao 98 na pasi za mabao 53.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment