Umiliki wa Liverpool waingia kwenye sura mpya


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Umiliki wa Liverpool umeingia katika hatua mpya baada ya Fenway Sports Group (FSG) kuuza karibu asilimia 40 ya hisa za klabu hiyo kwa muungano wa wawekezaji unaomjumuisha bilionea wa Marekani, Jeff Bezos.

Awali, taarifa zilieleza kuwa muungano huo umenunua kati ya asilimia 30 na theluthi moja ya hisa za Liverpool, hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa makubaliano hayo ni zaidi na kinafikia karibu asilimia 40.

Muungano huo unaojulikana kama 1892 Holdings unaongozwa na Amit Bhatia, ambaye aliwahi kuwa mmoja wa wamiliki wa Queens Park Rangers. Kupitia makubaliano hayo, muungano huo umepata takribani asilimia 38 ya hisa za Liverpool.

Mbali na umiliki huo, Bhatia anatarajiwa kuchukua nafasi ya makamu mwenyekiti wa Liverpool, hatua inayomuweka katika nafasi ya kushiriki moja kwa moja katika uongozi wa klabu.

Kwa upande mwingine, makubaliano kati ya 1892 Holdings na FSG yanaweka uwezekano wa wawekezaji hao kununua hisa za kudhibiti Liverpool ndani ya miezi 12 ijayo.

Hivyo, kinachobadilika si jina la mmiliki pekee, bali pia muundo wa umiliki wa Liverpool, FSG bado inaendelea kuwa sehemu ya umiliki wa klabu, wakati muungano huo ukipata nafasi kubwa kupitia ununuzi wa hisa.

Kwa Liverpool, hatua hii inaongeza kundi jipya la wawekezaji katika klabu ambayo imekuwa chini ya FSG tangu mwaka 2010.

0767915473,

lugembetimothy01@

gmail.com.

0/Post a Comment/Comments