Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, Concacaf na Shirikisho la Soka Asia (AFC) zimeendelea kusisitiza kuwa Gianni Infantino anapaswa kujiuzulu nafasi ya Rais wa FIFA.
Mashirikisho hayo matatu yalitoa barua ya pamoja ikiwa imesainiwa na marais pamoja na makatibu wakuu wa taasisi hizo, barua hiyo ilieleza ukosoaji wao dhidi ya uongozi wa Infantino na kutaka aondoke katika nafasi hiyo.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya FIFA kutoa taarifa iliyokosoa kile ilichokiita juhudi zinazoendelea za baadhi ya watu kumdhoofisha Infantino na taasisi hiyo.
Msimamo huo umeongeza mvutano kati ya FIFA na baadhi ya mashirikisho ya soka, huku UEFA, Concacaf na AFC zikiendelea kushikilia wito wao wa kutaka mabadiliko katika uongozi wa FIFA.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment