Udhamini wa Betting na wachezaji U-18


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Katika soka jezi imekuwa sehemu ya biashara inayoiunganisha klabu na wadhamini, nembo inayowekwa kwenye jezi inaweza kuwakilisha mkataba wa thamani kwa klabu, lakini uwepo wa wachezaji walio chini ya miaka 18 unaweka mipaka katika namna udhamini huo unavyoweza kuonekana.

Hilo limejitokeza wakati wa mchezo wa mzunguko wa pili NBC premier league kati ya Yanga dhidi ya coastal union kwenye uwanja wa KMC complex ambapo wananchi waliibuka na ushindi wa bao 4-1, mbali na ushindi huo Kuna hali ya utata ilitokea baada ya mchezaji wa Yanga Abdulnasiri (Casemiro) kuingia akitokea benchi akiwa amevalia jezi ambayo haina nembo ya mdhamini wa klabu hiyo "Sportpesa" tofauti na wachezaji wenzake.

Abdulnasiri Anamika 17 , kwa mujibu wa sheria za michezo ya kubahatisha nchini hazimruhusu mtu yoyote mwenye chini ya miaka 18 kujihusisha na michezo, matangazo au udhamini wa michezo ya kubahatisha , ndio maana mchezaji huyo alivalia jezi ambayo Haina mdgamini kutokana na kuwa chini ya umri unaonrihusiwa.

Hali kama hiyo imeonekana hivi karibuni England kwa kinda wa Manchester United JJ Gabriel mwenye miaka 15 ambapo Licha ya United kuwa na udhamini wa Betway kwenye vifaa vya mazoezi, Gabriel hakuruhusiwa kuvaa vifaa vyenye nembo ya kampuni hiyo kutokana na kuwa chini ya miaka 18 kwa mujibu wa sheria za EPL.

Mifano hiyo miwili inaonyesha namna soka linavyojaribu kuweka mipaka kati ya maslahi ya kibiashara ya klabu na ulinzi wa wachezaji chini yaiaka 18, Kwa Abdulnasir suala hilo lilionekana kwenye mchezo wa Yanga na Coastal Union, huku JJ Gabriel akiwa mfano wa namna utaratibu huo unavyoshughulikiwa katika soka la England.

Kwa hiyo, tofauti ya jezi ya Abdulnasir haikuwa suala la mavazi pekee, bali ni sehemu ya mjadala mpana kuhusu nafasi ya udhamini wa betting katika soka na namna wachezaji walio chini ya miaka 18 wanavyopaswa kuhusishwa nalo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments