Simanzi: Lionel Messi apoteza Baba

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Jorge Messi, baba wa Lionel Messi, amefariki dunia akiwa na miaka 68 baada ya kuugua kwa muda, huku familia yake ikiwa imekuwa ikifuatilia hali yake ya afya katika kipindi cha miezi kadhaa kabla ya kukutwa na umauti.

Jorge alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini na baadaye aliendelea na huduma nyumbani kwake mjini Rosario, Katika kipindi hicho, watoto wake Rodrigo, Matías na Maria Sol walifika kuwa karibu naye kwaajili ya uangalizi wa karibu.


Wakati huo, Lionel Messi aliendelea kuwasiliana na familia yake ili kupata taarifa kuhusu hali ya baba yake ambapo taarifa zinaeleza kuwa wakati mwingine hali yake ilionekana kuimarika, lakini baadaye ikaendelea kuwa mbaya.

Hali hiyo pia ilimfanya Messi kufikiria kuondoka kwenye mashindano ya kombe la Dunia ili kwenda kumuona baba yake hata hivyo, aliendelea na majukumu yake ndani ya timu ya taifa ya Argentina.

Baada ya kufunga bao dhidi ya Algeria, Messi alionekana akilia tukio ambalo lilikuwa miongoni mwa nyakati zilizodhihirisha hali aliyokuwa akipitia wakati huo ilikuwa ni ngumu.

Jorge alikuwa sehemu ya safari ya Messi katika soka, akihusika pia katika kusimamia mambo ya kazi ya mwanae tangu hatua za mwanzo za maisha yake ya kisoka mpaka anaiaga Dunia.

Kifo cha Jorge kimeacha familia ya Messi katika kipindi cha maombolezo, huku watu kutoka katika ulimwengu wa soka wakitoa salamu za pole kwa Lionel Messi na familia yake.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments