Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Ligi Kuu ya England (EPL) itaanza msimu wa 2026/27 ikiwa na mabadiliko ya sheria zinazolenga kudhibiti ucheleweshaji wa muda wakati wa mchezo na kufanya mchezo uchezwe kwa muda unaotakiwa.
Miongoni mwa mabadiliko hayo ni sheria inayomhusu mchezaji anayeumia akiwa ndani ya uwanja, Mchezaji anatakiwa kutoka nje ya uwanja na kukaa kwa angalau dakika moja kabla ya kuruhusiwa kurejea, badala ya sekunde 30 zilizokuwa zikitumika.
Aidha, Sheria hizo zimegusa sekunde tano za kuhesabu muda kwa mipira ya kurusha na mipira ya kuanzia golini, timu inapochelewesha kuanzisha mchezo baada ya mpira kuwa tayari kuchezwa, mwamuzi anaweza kuhesabu sekunde hizo na muda ukimalizika bila mchezo kuanzishwa, mpira utabadilishwa na kupewa timu pinzani kwa mujibu wa aina ya mpira uliokuwa ukisubiri kuchezwa.
Kwa upande wa mabadiliko ya wachezaji, mchezaji anayebadilishwa anatakiwa kutoka uwanjani ndani ya sekunde 10 ,akishindwa kufanya hivyo mchezaji anayetarajiwa kuingia hataruhusiwa kuingia hadi usimamishaji mwingine wa mchezo utakapotokea.
Mabadiliko mengine yanahusu matumizi ya VAR, Mfumo huo sasa unaweza kutumika kupitia uamuzi wa kadi ya pili ya njano endapo itaonekana kuwa mwamuzi alifanya kosa lililo wazi na kusababisha mchezaji kutolewa kwa kadi nyekundu.
Mabadiliko hayo yanaweka mkazo katika kupunguza muda unaopotea wakati wa mchezo, EPL sasa inaanza msimu ikiwa na utaratibu mpya wa kusimamia majeraha, mipira ya kuanzisha mchezo, mabadiliko ya wachezaji na baadhi ya maamuzi yanayohusisha VAR.
0767915473,
lugembetimothy01@
gmail.com.

Post a Comment