Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Golikipa wa Bayern Munich na timu ya Taifa ya Ujerumani, Manuel Neuer, ameendelea kuweka alama kwenye historia ya soka baada ya kufikisha jumla ya mataji 36 katika maisha yake ya soka.
Neuer, mwenye umri wa miaka 40, amefikia idadi hiyo kupitia mafanikio aliyoyapata akiwa na klabu, timu ya taifa. Kati ya mataji hayo, Neuer ametwaa Bundesliga mara 13, German Super Cup mara nane na DFB-Pokal mara sita. Mafanikio hayo yanaonyesha sehemu kubwa ya historia yake imejengwa akiwa Bayern Munich, ambako amekuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda mashindano mbalimbali.
Mbali na mafanikio ya ndani ya Ujerumani, Neuer pia ameshinda UEFA Champions League mara mbili, UEFA Super Cup mara mbili na FIFA Club World Cup mara mbili.
Katika ngazi ya timu ya taifa, Neuer alisaidia Ujerumani kushinda Kombe la Dunia la FIFA mara moja. Pia ana taji moja la UEFA European U21 Championship, huku akiwa amewahi kushinda DFL-Ligapokal mara moja.
Jumla hiyo ya mataji 36 inaweka jina la Neuer katika kundi la wachezaji waliokusanya vikombe vingi katika historia ya soka ujerumani ,rekodi hiyo pia inaonyesha namna alivyodumu katika kiwango cha juu kwa zaidi ya muongo mmoja.
Kwa Neuer, safari bado inaendelea, lakini idadi ya mataji aliyonayo tayari imeifanya sehemu ya historia yake kuandikwa kwa namba 36.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment