Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kocha wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho, amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa na subira na mshambuliaji raia wa Ivory Coast, Yan Diomandé, akisema mchezaji huyo anahitaji muda kuzoea maisha katika klabu hiyo.
Diomandé, mwenye umri wa miaka 19, amecheza mechi tatu za La Liga msimu huu akiwa akitokea benchi, akipata dakika 20, 15 na 30 za mchezo katika msimu huu.
Mchezaji huyo alijiunga na Real Madrid akitokea RB Leipzig kwaajili ya kwenda kuongeza nguvu katika kikosi hicho, jambo lililoongeza matarajio kwa kiwango chake tangu alipojiunga na klabu hiyo.
Hata hivyo, Mourinho amesema thamani ya uhamisho haipaswi kuwa sababu ya kumlazimisha Diomandé kuonyesha uwezo wake wote mara moja.
“Anahitaji kwenda hatua kwa hatua, amecheza dakika 20, 15 au 30 katika michezo mitatu hadi sasa anafanya kazi vizuri na kwa bidii. Ni mnyenyekevu, ana hamu ya kujifunza na kufanya kazi, Ananisikiliza mimi na wachezaji wenzake, Atakua,” alisema Mourinho.
Mourinho aliongeza kuwa Diomandé bado ni kijana na ana uwezo wa kuendelea kukua katika kikosi cha Real Madrid.
“Subira Kwa kawaida, watu wanapozungumza kuhusu kiasi kikubwa cha fedha, wanatarajia mchezaji aje na kutawala mara moja Hivyo sivyo ilivyo Yeye ni kijana sana, lakini ana uwezo mkubwa Muwe na subira,” alisema akiwaambia mashabiki wa timu hiyo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment