Mashabiki na hukumu ya kumzomea nyota wa timu

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezaji anapoingia uwanjani akiwa anajua kuwa mashabiki wake hawamtaki, mchezo unaweza kubadilika kabla hata mpira haujaanza, Zomea kutoka jukwaani zinaweza kumfanya mchezaji apoteze kujiamini, kucheza kwa presha na kuhisi kuwa hana tena nafasi ndani ya timu.

Katika soka, uhusiano kati ya mchezaji na mashabiki ni sehemu ya mazingira ya timu, Mashabiki wanapomuunga mkono mchezaji, humsaidia kupata morali na kujiamini anapokuwa uwanjani Lakini hali inapobadilika na mchezaji kuanza kuzomewa, athari zake zinaweza kuonekana kwenye uwanja kwa kiwango kushuka kutokana athari katika akili ya mchezaji.

Mchezaji anayekataliwa anaweza kuanza kufikiria zaidi kuhusu namna mashabiki watakavyopokea kila hatua yake kuliko kuzingatia mchezo, Kosa dogo linaweza kuongeza presha, huku kutokujiamini kukiathiri namna anavyocheza.na kusababisha kiwango kuporomoka.

Hali hiyo pia inaweza kuathiri timu, Mchezaji akiwa hana utulivu wa kiakili ushirikiano wake na wenzake unaweza kupungua na umakini wake ukahamia kwenye changamoto iliyo nje ya uwanja ndiyo maana migogoro kati ya mchezaji na mashabiki inaweza kuwa tatizo kwa klabu nzima na ikaathiri matokeo ya timu au mchezaji husika.


Mfano wa hali hiyo umejitokeza katika klabu ya Atletico Madrid, ambapo mshambuliaji Julian Alvarez alizomewa na mashabiki wa timu hiyo wakati wa mchezo wa LaLiga dhidi ya Villarreal kwenye Uwanja wa Metropolitano Mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Tukio hilo limetokea wakati ambapo Alvarez amekuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na Barcelona na Arsenal, Atletico Madrid haijawa tayari kumuachia kirahisi, lakini taarifa hizo zimeweka sintofahamu kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo ndani ya klabu.

Kutokana na hali hiyo , kumemuibua gwiji Zlatan Ibrahimovic ambaye amesharuri kuwa ni bora mchezaji kuondoka klabuni hapo kutokana na hali yaashabiki kutomuhitaji klabuni hapo, hata hivyo mpaka sasa klabu imesema kuwa Alvarez ataondoka klabuni hapo kwa Euro million 150.

Kwa mashabiki, mchezaji anapotaka kuondoka katika klabu wanayoipenda inaweza kuonekana kama ameamua kuweka mbele maslahi yake binafsi mara nyingine huonekana kama usaliti. Hisia hizo zinaweza kueleweka, lakini zomea za mara kwa mara zinaweza kumweka mchezaji katika mazingira ambayo si rahisi kwake kuendelea kutoa kiwango chake kwa klabu.

Kwa klabu, changamoto huwa ni kuhakikisha kuwa tofauti kati ya mchezaji na mashabiki hazivurugi kazi ya timu, Mchezaji anaweza kuwa na nia ya kuondoka, lakini bado anahitajika kuitumikia timu hadi pale uhamisho utakapokamilika.

Kwa hiyo, katika soka, kutaka kuondoka kwenye klabu si mwisho wa uhusiano kati ya mchezaji na klabu, Lakini namna suala hilo linavyoshughulikiwa inaweza kuamua kama mchezaji ataendelea kuwa sehemu ya timu au uhusiano wake na mashabiki utavunjika kabla hata ya kuondoka.


Ikumbukwe kuwa mchezaji kuondoka kwenye klabu haimaanishi anajitenga na familia hiyo Bali anaenda kutafuta changamoto nyingine na baadae anaweza kurejea kwa mara nyingine kulitumikia timu hiyo wakati anataka kustaafu kama shujaa wa timu , kwa Tanzania mfano ni Chama na Luis Miqusone wachezaji walio ondoka Simba wakiwa Bado wanahitahila lakini waliondoka kwa heshima lakini baadae walirejea kwenye timu, hiyo yote ni kutokana na uhusiano bora waliyokuwa nayo na mashabiki.

Mbali na Tanzania, mfano mwingine ni Christiano Ronaldo ambaye alikuwa nyota kwenye klabu ya Manchester United, aliondoka kutimkia Real Madrid lakini alirejea Tena baadae kutumikia timu hiyo yote hiyo ni kutokana na heshima ya mashabiki kwa mchezaji.

Chakuzingazia niashabiki kuelewa kuwa mpira ni ajira kama ajira nyingine na maamuzi ya mchezaji yanatakiwa kuheshimiwa, na mchezaji kuondoka klabuni hakutakuwi kuvunja uhusiano kati ya mashabiki na mchezaji au klabu na mchezaji.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments