Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kombe la Dunia limeendelea kubadilika kadri soka linavyopanuka ulimwenguni, Kila toleo huleta mabadiliko yanayolenga kuongeza ushindani, ushiriki wa mataifa na mvuto wa mashindano. Toleo la mwaka 2026 limeingia katika historia kwa kuanzisha mfumo mpya ambao haujawahi kutumika tangu mashindano hayo yalipoanza mwaka 1930.
Tofauti kubwa ni ongezeko la timu zinazoshiriki, Kwa mara ya kwanza, Kombe la Dunia limehusisha timu 48 badala ya 32 zilizotumika kuanzia mwaka 1998 hadi 2022 mabadiliko hayo yameongeza nafasi kwa mataifa mengi kufuzu kwenye mashindano hayo, FIFA imeeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza ushiriki na kutoa nafasi kwa mataifa zaidi kushiriki jukwaa hilo la kimataifa.
Mbali na idadi ya timu, mashindano hayo yameandaliwa kwa mara ya kwanza na nchi tatu kwa pamoja ambazo ni Marekani, Canada na Mexico. Mfumo huo umeongeza idadi ya miji na viwanja vinavyotumika, huku ukihitaji maandalizi makubwa ya usafiri, usalama na uratibu wa ratiba za timu na mashabiki.
Mabadiliko mengine yameonekana kwenye mfumo wa mashindano, timu 48 zimegawanywa katika makundi 12 yenye timu nne kila kundi na timu mbili za juu kutoka kila kundi pamoja na timu nane bora zilizomaliza nafasi ya tatu zinafuzu hatua ya 32 bora, mfumo huo umeongeza hatua moja ya mtoano kabla ya hatua ya 16 bora, jambo lililoongeza idadi ya michezo kutoka 64 hadi 104.
Mbali na hayo, Kuna kitu kipya kingine kilichofanyika katikati ya mchezo "Hydration break" , hii ilitokea kwenye vipindi vyote viwili ambapo timu zilipata muda wakupata maji na mawaidha kutoka kwa waalimu wao kwa dakika chache kabla ya kuendelea na mchezo.
Matumizi ya sayansi na teknolojia nayo yalichukuwa nafasi katika mashindano hayo, mpira uliotumika katika mashindano hayo "traonda" ulikuwa wa kitofauti kutokana na namna ulivyo tengenezwa, mpira ulichajiwa badala ya kujazwa upepo pia ulifungwa kifaa maalumu ambacho kilinusa Kila mguso wa mpira na kuwarahisishia waamuzi kazi.
Hata hivyo, mfumo huo mpya unaambatana na changamoto, Kuongezeka kwa michezo kunamaanisha ratiba ndefu zaidi, safari nyingi kati ya miji na nchi tatu, pamoja na ongezeko la mzigo kwa wachezaji.
Kwa ujumla, Kombe la Dunia 2026 limefungua ukurasa mpya katika historia ya soka, Ongezeko la timu, mfumo mpya wa mashindano , ushirikiano wa nchi tatu wenyeji na matumizi makubwa ya teknolojia ni mabadiliko yanayoonyesha namna mashindano hayo yanavyoendelea kuwa na mabadiliko.
0767915473
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment