Kwa nini kipa huvaa jezi yenye rangi tofauti na wachezaji wengine?


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Katika mchezo wa soka, kipa hutambulika kwa jambo moja linaloonekana wazi uwanjani, jezi yake huwa na rangi tofauti na zile zinazovaliwa na wachezaji wengine, tofauti hii si suala la muonekano bali ni matakwa ya Sheria za Mchezo wa Soka.

Kwa mujibu wa Sheria ya 4 ya IFAB inayohusu vifaa vya wachezaji, kipa anatakiwa kuvaa rangi inayomtenganisha na wachezaji wengine, kipa wa timu pinzani na waamuzi, Kanuni hii imewekwa ili kipa aweze kutambulika kwa urahisi wakati wa matukio mbali mbali ndani ya mchezo.

Kipa ana jukumu tofauti na wachezaji wengine akiwa kwenye eneo lake la penalti ambapo anaruhusiwa kutumia mikono katika mazingira yanayoruhusiwa na sheria. Hivyo, kumtambua kipa kwa haraka ni muhimu kwa wachezaji na waamuzi wakati mchezo.

Hata hivyo, Wakati wa shambulizi, mpira wa kona, mpira wa adhabu au hali nyingine inayotokea karibu na lango, wachezaji wanapaswa kujua mara moja ni nani mwenye nafasi ya kipa ili kurahisisha namna ya mchezo unavoenda , rangi tofauti kwenye jezi hufanya utambuzi huo kuwa rahisi bila kutegemea namba ya jezi au sura ya mchezaji.

Kanuni hiyo pia inahakikisha kuwa kipa hatambuliki kwa kuchanganywa na mwamuzi, Waamuzi wana mavazi yao maalum, hivyo rangi ya jezi ya kipa inapaswa kuwa tofauti na mavazi yao, Vilevile, inapowezekana, makipa wa timu mbili wanapaswa kuvaa rangi zinazotofautiana.


Hata hivyo, sheria inatambua kuwa kuna mazingira ambayo tofauti hiyo inaweza kushindikana hivyo Ikiwa makipa wawili wana jezi zinazofanana na hakuna uwezekano wa kupata jezi nyingine, mwamuzi anaweza kuruhusu mchezo kuendelea, lengo la msingi si kulazimisha mabadiliko ya jezi kwa gharama ya kusimamisha mchezo, bali kuhakikisha utambulisho wa kipa unafanyika.

Kwa hiyo, rangi tofauti ya jezi ya kipa ni muhimu ambapo kumtambulisha kipa kwa haraka na kumtofautisha na wachezaji wengine pamoja na waamuzi.

Hivyo, kile kinachoonekana kama tofauti ya kawaida ya mavazi ni sehemu ya utaratibu wa sheria za soka, Kila kipa anapoingia uwanjani akiwa na jezi ya rangi tofauti, anakuwa ametekeleza moja ya matakwa ya vifaa vya wachezaji yaliyowekwa na IFAB (International Football Association Board).

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments