Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Uongozi wa Klabu ya Simba umesema kikao kilichofanyika Bunju, Dar es Salaam, Agosti 2, 2026 hakikuwa Mkutano Mkuu Maalum wa wanachama, hivyo maamuzi yoyote yaliyotolewa katika kikao hicho hayana uhalali wa kikatiba.
Taarifa hiyo imelenga kutoa ufafanuzi kuhusu hadhi ya kikao hicho na kueleza kuwa Mkutano Mkuu Maalum wa wanachama unaweza kufanyika tu baada ya kufuatwa taratibu zilizoainishwa kwenye katiba ya klabu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori, Katiba ya Simba ya mwaka 2018 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2026 inaeleza kuwa Mkutano Mkuu Maalum huitishwa na Mwenyekiti wa Klabu kwa kushirikiana na Bodi ya Wakurugenzi.
Wakati huohuo, uongozi wa Simba umeeleza kuwa Agosti 3, 2026 Bodi ya Wakurugenzi itafanya kikao cha kujadili ajenda zitakazowasilishwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa wanachama kabla ya kutangaza rasmi tarehe ya mkutano huo.
Kutokana na hatua hiyo, klabu imewataka wanachama kuendelea kufuata taratibu za katiba na kusubiri taarifa rasmi zitakazotolewa na vyombo vya uongozi kuhusu mchakato wa kuitishwa kwa Mkutano Mkuu Maalum.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment