Kelele za mashabiki za ibua changamoto za msongo wa mawazo kwa mchezaji


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, ameripotiwa kuwasilisha taarifa ya kitabibu kwa klabu hiyo baada ya kukumbwa na changamoto ya msongo wa mawazo (depression) huku hali yake ikiibuka siku chache baada ya kuzomewa na mashabiki wa klabu yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya kituo kimoja Cha redio nchini Hispania , Alvarez amegundulika kuwa na depression na amewasilisha nyaraka za kitabibu kwa klabu, Hata hivyo, klabu hiyo haijatoa taarifa rasmi kuthibitisha madai hayo.Taarifa hiyo imekuja baada ya mchezaji huyo kuzomewa na mashabiki wa Atletico katika mchezo wa LaLiga dhidi ya Villarreal uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Kuzomewa huko kumetokea wakati kukiwa na mvutano kuhusu mustakabali wa Álvarez, ambaye amehusishwa na uwezekano wa kuondoka Atlético Madrid huku Barcelona ikionyesha nia ya kumsajili, lakini Atletico imesema haitafanya mazungumzo na klabu hiyo kuhusu uhamisho wake.

Hivyo kwa kinacho endelea kwa mchezaji , uamuzi sahihi unaotakiwa kufanywa ni kumruhusu kuondoka klabuni na kujiunga na klabu nyingine ambako atakuwa na furaha kuliko kumkumbatia na kutokuwa na manufaa kwa klabu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments