Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Afya ya mwili haianzii gym wala jikoni pekee, huanzia kwenye lishe na mchakato mzuri wa mazoezi ya mwili ndiyo maana chakula na mazoezi huenda sambamba.
Chakula ndicho chanzo cha nishati ya mwili kwa shughuli za kila siku kama kutembea, kazi na mazoezi, aina ya chakula huathiri moja kwa moja utendaji wa mwili.
Mwili huhitaji virutubisho mbalimbali kama vile wanga kwa nishati, protini kwa ujenzi wa misuli, mafuta kwa kazi muhimu, na matunda pamoja na mboga kwa vitamini na madini. Baada ya chakula, mazoezi kama kutembea, kukimbia au kuogelea husaidia mwili kutumia nishati na kuuweka katika hali ya afya iliyo bora
Mazoezi huimarisha misuli na mifupa pia husaidia udhibiti wa uzito na kuboresha uwezo wa kufanya shughuli za kila siku huku miwili ukiwa wenye afya.
Chakula na mazoezi hutegemeana kwa kiasi kikubwa kwani Kula bila mazoezi au mazoezi bila lishe bora huleta usawa mbaya wa mwili, Kwa mfano, mazoezi bila lishe ya kutosha hupunguza nguvu, na kula kupita kiasi bila mazoezi huongeza uzito.
Maji pia ni muhimu, hasa wakati wa mazoezi kwani hupotea kupitia jasho na yanahitajika pia baada ya mazoezi ili kufanya miwili uendelee na kazi zake.
Kwa ujumla, afya hujengwa na tabia endelevu ya lishe bora, mazoezi na unywaji wa maji wa kutosha, chakula hutoa nishati, mazoezi huiweka mwili hai, na vyote viwili ni muhimu kwa maisha yenye afya bora.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment