Bayern Yaweka Imani kwa Musiala, Yakataa Kusajili Mbadala Wake

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Changamoto ya kiafya ya Jamal Musiala imeiweka Bayern Munich kwenye hali ambayo inahitaji klabu kufanya maamuzi kuhusu namna ya kuendelea bila mchezaji huyo, huku uamuzi wa sasa ukiwa ni kutosajili mchezaji mwingine wa kuziba nafasi yake.

Musiala (23) amekuwa akipitia tatizo la kiafya lililohusisha kutokea kwa vipindi vifupi vya kupoteza fahamu, hali ambayo imeelezwa kusababishwa na hitilafu katika mfumo wa wake wa neva, hata hivyo, mchezaji huyo amesema yuko chini ya uangalizi wa wataalamu na anaendelea na matibabu.

Katika ujumbe wake, Musiala amesema anaelewa hofu iliyojitokeza miongoni mwa mashabiki na watu wanaomfuatilia, ameeleza kuwa hali hiyo ni sehemu ya maisha yake kwa sasa na kwamba anaendelea na matibabu huku akiwa na matumaini ya kuendelea na maisha ya kawaida pamoja na soka.

Zaidi ya hapo, amesema Bayern Munich pamoja na watu wake wa karibu wameendelea kuwa sehemu ya safari yake ya kupona na Kwa mujibu wa maelezo yake, amekuwa akishirikiana na wataalamu wa afya na ameamua kuelekeza nguvu katika mambo yanayomsaidia kuendelea na maisha na kurejea kwenye shughuli za soka.


Pamoja na hali hiyo, Bayern Munich haijaweka mpango wa kumsajili mchezaji mwingine kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Musiala, Klabu hiyo imeamua kumpa muda na kuendelea kumuunga mkono wakati akifuatilia matibabu yake.

Badala ya kufanya usajili wa haraka, Bayern inaangalia wachezaji waliopo ndani ya kikosi ambao wanaweza kutumika katika nafasi ya namba 10, Miongoni mwao ni Lennart Karl, Ismael Saibari na Serge Gnabry.

Uamuzi huo unaonyesha namna Bayern inavyopanga kuendelea na msimu huku ikimsubiri Musiala arejee kwenye ubora wake, Klabu haioni ulazima wa kuongeza mchezaji mwingine kwa sasa, kutokana na uwepo wa chaguo ndani ya kikosi.


Kwa upande wake, Musiala amesema anaendelea kuwa na mtazamo wa kurejea kwenye maisha yake ya kawaida na kuendelea na soka, pia ameomba kuwa jambo hilo libaki zaidi kati yake, watu wake wa karibu, klabu na wataalamu wanaomsaidia.

0757915473,

lugembetimothy01

@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments