Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Barcelona imepiga hatua katika harakati za kumsajili kiungo wa Hispania na klabu ya Man City Rodri baada ya mchezaji huyo kukubali masharti binafsi ya mkataba yaliyowasilishwa na timu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rodri ameonyesha nia ya kujiunga na Barcelona, hatua inayowapa viongozi wa klabu hiyo nafasi ya kuanza mazungumzo rasmi na Manchester City kuhusu ada ya uhamisho wake.
Rodri amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa Manchester City katika misimu ya hivi karibuni , nyota huyo ameendelea kuwa sehemu ya kikosi cha City baada ya kurejea uwanjani kufuatia kipindi alichokosa kutokana na majeraha. Uwepo wake umeongeza utulivu katika safu ya kiungo kutokana na uwezo wake wa kukaba, kuanzisha mashambulizi na kudhibiti kasi ya mchezo.
Mbali na mafanikio yake ndani ya klabu, Rodri ni mshindi wa Kombe la Dunia 2026 akisindikizwa na tuzo ya mchezaji bora wa mashindano, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu England pia mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or ya mwaka 2024, mafanikio yaliyomweka miongoni mwa viungo bora duniani.
Barcelona sasa inatarajiwa kuanza mazungumzo na Manchester City ili kufikia makubaliano ya mwisho kuhusu uhamisho huo, hata hivyo, City bado haijatoa tamko rasmi kuhusu hatma ya nyota huyo huku mazungumzo yakitarajiwa kuendelea katika siku zijazo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment