Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshindi wa Ballon d’Or mwaka 2005, Ronaldinho, amerejea kwenye soka la ushindani akiwa na miaka 46 baada ya kukaa nje ya mchezo huo kwa miaka 11, akijiunga na Ravenna inayoshiriki Serie C nchini Italia.
Ronaldinho aliwasili Italia Alhamisi na kutambulishwa mbele ya mashabiki wa Ravenna, Usajili wake ulitangazwa Juni, lakini sasa ameingia rasmi kwenye mpango wa klabu hiyo kama mwekezaji na mchezaji anayeweza kushuka dimbani.
Mchezo wake wa mwisho wa ushindani ulikuwa mwaka 2015 akiwa na Fluminense, kabla ya kustaafu soka mwaka 2018, baada ya miaka 11 bila kucheza mchezo rasmi, sasa ana nafasi ya kurejea uwanjani akiwa na Ravenna.
Lengo la Ronaldinho ni kucheza angalau mchezo mmoja na kujaribu kufunga bao la 300 katika maisha yake ya soka, Rais wa Ravenna, Ignazio Cipriani, amesema nia ya klabu ni kumuona Mbrazil huyo akifunga bao la mwisho la taaluma yake akiwa na timu hiyo.
Hata hivyo, Ronaldinho hatacheza katika mchezo wa kwanza wa Ravenna dhidi ya Reggiana. Muda wa kurejea kwake uwanjani bado haujawekwa wazi, huku uamuzi wa kumpanga ukitegemea benchi la ufundi na uongozi wa klabu.
Mbali na kucheza, Ronaldinho amekuwa mmoja wa wanahisa wa Ravenna, huku klabu hiyo ikiwa na mpango wa kupanda hadi Serie B baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika Kundi B la Serie C msimu uliopita.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment