Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Matumizi ya teknolojia ya FVS katika Ligi Kuu Tanzania Bara yatafanyika kwa asilimia 70 katika hatua ya mwanzo, hivyo si kila mchezo utatumia teknolojia hiyo.
Kwa mujibu wa TFF wakati teknolojia hiyo ilipotambulishwa rasmi, matumizi yake yamepangwa kwa kiwango hicho kutokana na kuwa bado ni hatua ya kwanza ya utekelezaji na majaribio, hivyo, mashabiki na wadau wa soka hawapaswi kushangaa kuona baadhi ya michezo ikiendelea bila kutumia FVS.
Kama kutakuwa na mchezo unaohusisha timu kubwa ambao hautatumia teknolojia hiyo, hali hiyo haimaanishi kuwa kuna mkakati maalum bali ni sehemu ya mpangilio wa matumizi ya FVS katika hatua hii ya awali.
Kutumika kwa asilimia 70 bado ni hatua katika kuanza kuingiza teknolojia hiyo kwenye ligi, Kadri matumizi yatakavyoendelea na mfumo kuimarika, lengo ni kufikia asilimia 100 ili michezo yote iweze kunufaika na teknolojia hiyo.
Hatua hiyo pia inalenga kuongeza usawa katika maamuzi ya waamuzi na kuendelea kuifanya Ligi Kuu Tanzania Bara kuwa na mfumo unaoendana na mabadiliko ya teknolojia katika soka.
Kwa hiyo, kutokuwepo kwa FVS katika mchezo fulani hakupaswi kutafsiriwa kama upendeleo au mkakati dhidi ya timu yoyote, bali ni utekelezaji wa mpango uliowekwa kwa awamu
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment