Arsenal waanzia walipoishia wakifikisha Ngao ya 18

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Arsenal wameanza msimu wa 2026/27 kwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Manchester City mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Principality, Cardiff nchini Wales siku ya agosti 16, 2026.

Riccardo Calafiori alifungua ukurasa wa mabao, kabla ya Kai Havertz kuongeza la pili na Martin Ødegaard kukamilisha ushindi huo, Mabao hayo yaliifanya Arsenal kuanza msimu wakiwa na taji huku wakivunja rekodi nyingine katika historia ya Ngao ya Jamii.

Taji hili linakuwa la 18 kwa Arsenal katika ngao ya jamii , hivyo kuwa klabu pili kwa idadi kubwa ya taji hilo huku Manchester United ikiongoza ikiwa na mataji 21.

Mafanikio hayo yanaingia katika kipindi ambacho Arsenal wameanza kurejea kwenye nafasi ya ushindani wa juu chini ya kocha Mikel Arteta baada ya kusubiri kwa takribani miaka 20 bila kutwaa Ligi Kuu, Arsenal walifanikiwa kushinda ubingwa msimu uliopita wa 2025/26.


Sasa wameanza msimu mpya kwa taji lingine, jambo linaloipa timu hiyo msingi wa kuendelea na mwenendo ulioanza kuonekana katika misimu ya hivi karibuni.

Chini ya Arteta, Arsenal wamekuwa wakijenga kikosi kinachoshindana mara kwa mara katika kilele cha Ligi Kuu, Ngao ya Jamii inaweza kuwa hatua ya kwanza katika msimu ambao wanatafuta kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu.

Kwa sasa, Arsenal wanaanza msimu wa 2026/27 wakiwa na rekodi ya Ngao ya Jamii mikononi mwao na taji la 18 la mashindano hayo katika historia ya klabu huku wakiwa kwenye mbio za kuandika ubingwa mwingine wa EPL.

0767915473,

lugembetimothy01@

gmail.com.

0/Post a Comment/Comments