Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kuna wakati historia haijengwi kwa kubeba kombe pekee bali kwa kufungua mlango ambao haujawahi kufunguliwa , ndivyo ilivyo kwa Yaya Touré, ambaye ameanza kuandika ukurasa mpya katika safari ya makocha wa Afrika baada ya kuipeleka Slovan Bratislava kwenye league phase ya UEFA Champions League.
Touré amekuwa Mwafrika wa kwanza kufikisha timu kwenye hatua hiyo akiwa kocha mkuu, baada ya kuiongoza Slovan kuvuka mchujo wa Champions League msimu wa 2026/27. Slovan ilifikia hatua hiyo baada ya kuiondoa NK Celje ya Slovenia kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza, Slovan ilishinda 2-1 katika mchezo wa pili uliokwenda hadi muda wa ziada, na kupata tiketi ya league phase.
Mafanikio hayo yanamuweka Touré kwenye nafasi tofauti katika historia ya soka la Afrika ambapo Makocha kutoka bara hilo wamewahi kuongoza klabu katika Champions League, lakini Touré ndiye aliyefikisha timu kwenye league phase kupitia hatua za mchujo mpaka UEFA phase league (36 Bora) akiwa kocha mkuu.
Kwa Touré, hii ni sura nyingine ya maisha yake ya soka, akiwa mchezaji, alishinda Champions League akiwa na Barcelona mwaka 2009 baada ya kustaafu kucheza, alianza safari ya ukocha akiwa katika nafasi mbalimbali za benchi la ufundi kabla ya kupata nafasi ya kuiongoza Slovan Bratislava.
Sasa anarejea Champions League akiwa upande wa benchi, lakini safari hii akiwa na jukumu la kupanga na kuiongoza timu ndani ya uwanja.
Slovan Bratislava itakutana na baadhi ya klabu kubwa za Ulaya katika hatua hiyo, huku Touré akiwa ameshafanikisha jambo ambalo hakuna kocha Mwafrika aliyewahi kulifanya kabla yake.
Kwa hiyo, hata kabla ya kucheza mchezo wake wa kwanza kwenye league phase, Touré tayari ameweka alama yake katika historia ya soka la Afrika.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment