2026 hatima kwa wafalme wa soka Dunia


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mwaka 2026 unaonekana kama mwaka wa mabadiliko katika soka la dunia, baada ya baadhi ya mastaa waliotawala mchezo huo kwa miaka mingi kwa vipaji na ubora wao kuanza kufunga milango ya safari zao kwa kutoa matamko nayayo ashiria mwisho wa zama zao.

Miongoni mwao ni Cristiano Ronaldo, mwenye miaka 41, ambaye ameashiria kuwa msimu huu unaweza kuwa wa mwisho kwake katika soka la kulipwa, Katika mahojiano na Vogue, Ronaldo alisema mwaka huu huenda ukawa mwisho wa safari yake uwanjani na kwamba anataka kuondoka akiwa ameacha urithi mkubwa.


Kauli hiyo haikuwa tangazo rasmi la kustaafu, lakini imeweka wazi kuwa Ronaldo, ambaye amekuwa kwenye soka la kiwango cha juu kwa zaidi ya miaka 20, sasa yupo katika hatua za mwisho za kazi yake.

Kabla , Neymar Jr baada ya Brazil kuondolewa katika Kombe la Dunia 2026, alitangaza kuwa hatacheza tena timu ya taifa, Neymar mwenye miaka 34 alimaliza safari yake ya kimataifa akiwa mfungaji bora wa Brazil kwa mabao 80 katika mechi 130.


Kwa Lionel Messi, bado hakuna tangazo la kustaafu, lakini kifo cha baba yake, Jorge Messi, kimeibua mashaka kuhusu mustakabali wake, Messi ameeleza kuwa ana maswali mengi kuhusu kuendelea kucheza soka kwa muda mrefu baada ya kumpoteza mtu aliyekuwa sehemu muhimu ya maisha na safari yake ya soka.


Hivyo, 2026 si mwaka wa mashindano pekee, bali pia ni kipindi ambacho kizazi cha Ronaldo, Messi na Neymar kinaanza kuonekana kikielekea mwisho wa safari, wachezaji hao Waliotawala soka kwa miaka mingi sasa wanaacha nafasi kwa kizazi kingine kuandika historia yao.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments