ZIDANE KUKABIDHIWA TIMU YA TAIFA YA UFARANSA BAADA YA KOMBE LA DUNIA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Zinedine Zidane anatarajiwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Ufaransa baada ya Didier Deschamps kumaliza majukumu baada ya Kombe la Dunia la 2026, hatua inayotarajiwa kufungua ukurasa mpya kwa mabingwa hao wa dunia wa mwaka 2018. 

Deschamps, ambaye ameinoa Ufaransa tangu mwaka 2012, anaondoka baada ya kuitumikia timu hiyo kwa zaidi ya muongo mmoja. Katika kipindi chake aliiongoza Ufaransa kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2018, kufika fainali ya mwaka 2022 na kutwaa pia taji la UEFA Nations League mwaka 2021, huku akiijenga timu iliyobaki miongoni mwa vigogo wa soka la kimataifa. 

Baada ya Ufaransa kuondolewa na Hispania katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026, safari ya Deschamps inaelekea kutamatika mara baada ya kuchezo mchezo wa mshindi wa tatu wa mashindano hayo, huku macho yakielekezwa kwa Zidane ambaye ametajwa kwa muda mrefu kuwa mrithi wake. 

Zidane, aliyewahi kuiongoza Real Madrid kutwaa mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, anatarajiwa kukabidhiwa jukumu la kuiongoza Ufaransa kuelekea Euro 2028 na maandalizi ya Kombe la Dunia 2030. Ingawa Shirikisho la Soka la Ufaransa halijatangaza rasmi uteuzi huo, taarifa mbalimbali zinaeleza kuwa makubaliano ya kumkabidhi mikoba hiyo tayari yamefikiwa. 

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments