WASIFU WA ALBERT KANGWANDA NYOTA ALIE MWAGA WINO JANGWANI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

 Klabu ya Yanga SC imekamilisha taratibu za kumsajili mshambuliaji Albert Kangwanda kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya msimu wa mashindano wa 2026/2027.

Mchezaji huyo raia wa Zambia anajiunga na Yanga akitokea klabu ya Red Arrows ya nchini kwao Katika msimu wa 2025/2026, mshambuliaji huyo amecheza jumla ya michezo 25, ambapo alifunga mabao 11 na kutoa pasi mbili za mabao, akihusika katika jumla ya mabao 13.

Kabla ya kutua Yanga, Kangwanda amewahi kucheza katika klabu nyingine zikiwemo Al Hilal Omdurman ya Sudan pamoja na HNK Gorica inayoshiriki ligi kuu ya nchini Croatia.

Wasifu wa Mchezaji:

Tarehe ya Kuzaliwa: 07/04/1998

Umri: Miaka 27

Nafasi: Winga wa Kulia / Mshambuliaji

Utaifa: Zambia

Usajili huu unalenga kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuelekea mashindano ya ndani na kimataifa kwa msimu ujao

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com







0/Post a Comment/Comments