VITA YA UBINGWA KATI YA SENEGAL NA MOROCCO KUAMULIWA OKTOBA 8, 2026

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imepanga kusikiliza rufaa kuhusu ubingwa wa Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) tarehe 8 Oktoba 2026 , hatua ambayo inatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho juu ya mgogoro unaozihusisha timu za Senegal na Morocco.

Mgogoro huo ulianza baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuamua kuwapokonya ubingwa Senegal baada ya timu hiyo kugomea mchezo na kutoka nje ya uwanja wakipinga maamuzi ya mkwaju wa penati waliopatiwa wapinzani wao na baadae walirudi uwanjani huku mchezo ukitamatika kwa Senegal kushinda 1-0, jambo hilo lililalamikiwa na Morocco na kuwasilisha lalamiko lao na CAF wakachukua maamuzi ya kuwapa ubingwa Morocco kwa ushindi wa mezani wa goli 3-0 

Hata hivyo, Shirikisho la Soka la Senegal halikukubaliana na uamuzi huo na kuwasilisha rufaa CAS, likitaka uamuzi wa CAF upitiwe upya kwa kuaminika kuwa ubingwa waliopokonywa wanastahili 

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, pande zote zitapata nafasi ya kuwasilisha hoja zao mbele ya mahakama hiyo kabla ya kutolewa kwa uamuzi wa mwisho.

Matokeo ya usikilizwaji huo yataamua iwapo ubingwa utaendelea kubaki Morocco au kama kutakuwa na mabadiliko kufuatia uamuzi wa CAS, hivyo bingwa halali wa AfCON2025 atajulikana rasmi baada ya kikao Cha pamoja Oktoba 8, 2026.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments