VIATU VIMETEMBEA WAKATI UFARANSA IKITINGA ROBO FAINALI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026 kati ya Paraguay na Ufaransa umeacha mjadala mkubwa kutokana na namna ulivyochezwa na maamuzi kwa baadhi ya matukio wakati wa mchezo.

Paraguay ilimaliza mchezo huo ikiwa imefanya faulo 13, lakini haikuonyeshwa hata kadi moja ya njano, hali hiyo imezua maswali kwa mashabiki na wadau wa soka, hasa kwa kuwa mchezo ulikuwa na vipindi vingi vya faulo na kusimamishwa mara kwa mara.

Badala yake, Ufaransa ndiyo iliyopata kadi tatu za njano, jambo lililoongeza mjadala kuhusu namna mwamuzi alivyosimamia mchezo huo. Kwa sehemu kubwa ya mchezo, Paraguay ilicheza kwa nguvu na kujaribu kuvuruga mpangilio wa wapinzani wao, mtindo ambao mara nyingi huonekana kwa baadhi ya timu za Amerika Kusini.

Licha ya presha hiyo, Ufaransa ilifanikiwa kushinda kwa bao 1-0 na kutinga hatua ya robo fainali ambapo watavaana na Morocco. Hata hivyo, mbali na ushindi huo, jambo lililobaki kwenye mjadala ni Paraguay kumaliza dakika 90 za mchezo ikiwa na faulo 13 bila kupewa kadi yoyote.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.





0/Post a Comment/Comments