Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Rais wa Barcelona, Joan Laporta, amesema klabu hiyo haina mpango wa kumuuza winga wa Brazil, Raphinha, katika dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi licha ya kuwapo kwa ofa kutoka klabu za Saudi Arabia.
Laporta amesema Raphinha anaendelea kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Barcelona, akisisitiza kuwa klabu inaendelea kumtegemea kuelekea msimu mpya.
"Hatutaki Raphinha aondoke, Ni mchezaji muhimu sana kwetu."alisema
Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na taarifa za Barcelona Kuwasajili nyota Anthony Gordon na Karim Adeyemi, jambo lililozua uvumi kuwa mmoja wa wachezaji wa safu ya ushambuliaji angeweza kuondoka.
Hata hivyo, Laporta ameeleza kuwa usajili wa Gordon na Adeyemi hauhusiani na mustakabali wa Raphinha, hivyo mashabiki hawapaswi kutafsiri hatua hiyo kama ishara ya kuondoka kwa nyota huyo.
"Usajili wa Anthony Gordon na Adeyemi hauhusiani na Raphinha, haimaanishi kwamba Rapha anaondoka." Aliongeza.
Raphinha amebaki kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuendelea kuiongoza Barcelona katika kampeni za msimu ujao, huku uongozi wa klabu ukionyesha dhamira ya kuendelea kumjumuisha katika mipango yake ya msimu ujao.
0767815473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment