Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mvutano kati ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) umechukua mwelekeo mpya baada ya taarifa kueleza kuwa vyama vyote 55 wanachama wa UEFA vinajadili uwezekano wa kususia baadhi ya mashindano yanayoandaliwa na FIFA, ikiwemo Kombe la Dunia.
Hatua hiyo inatajwa kuhusishwa na mpango wa Rais wa FIFA, Gianni Infantino, wa kuruhusu wawekezaji binafsi kununua hisa katika shughuli za kibiashara zinazohusiana na Kombe la Dunia.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, mazungumzo bado yanaendelea ndani ya UEFA na hakuna uamuzi rasmi ambao umeidhinishwa na vyama vyote 55 ambao ni wanachama wake.
Iwapo pendekezo hilo litapitishwa, linaweza kuathiri uhusiano kati ya UEFA na FIFA pamoja na mwenendo wa mashindano ya kimataifa katika miaka ijayo.
Wakati huohuo, pande hizo mbili zinaendelea kutofautiana kuhusu namna ya kusimamia na kuendeleza mashindano ya soka duniani, huku mjadala ukihusu pia ushiriki wa sekta binafsi katika shughuli za kibiashara zinazohusiana na Kombe la Dunia.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment