Twiga Stars yaanza WAFCON kwa ushindi, yaweka matumaini ya kufuzu Kombe la Dunia 2027

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya Taifa ya wanawake Tanzania, Twiga Stars, imeanza kampeni ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi B uliochezwa nchini Morocco.

Ushindi huo umeipa Tanzania alama tatu katika hatua ya makundi na kuongeza nafasi ya kuwania kufuzu hatua inayofuata ya mashindano hayo.

Kupitia WAFCON 2026, timu zitakazofika hatua ya nusu fainali zitapata nafasi ya kushiriki moja kwa moja fainali za Kombe la Dunia la Wanawake 2027 zitakazofanyika nchini Brazil.

Twiga Stars imepangwa Kundi B pamoja na Afrika Kusini, Burkina Faso na Ivory Coast, huku michezo iliyobaki ya hatua ya makundi ikiwa dhidi ya Burkina Faso Julai 31, na Ivory coast Agosti 4 , 2026 , wakihitaji angalau alama tatu kujihakikishia kufuzu hatua inayo fuata.

Mafanikio wanayoendelea kupata Twiga stars yanakuja baada ya uwekezaji unaoendelea katika soka la wanawake nchini Tanzania kupitia ligi ya wanawake na programu mbalimbali za maendeleo ya wachezaji.

Twiga Stars sasa itaendelea na maandalizi kwa michezo inayofuata ikiwa na lengo la kumaliza hatua ya makundi katika nafasi itakayoiwezesha kufuzu hatua ya mtoano na kuendelea kusaka nafasi ya kucheza Kombe la Dunia la Wanawake 2027.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com






0/Post a Comment/Comments