Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports
Rais wa Marekani, Donald Trump, ameizungumzia timu ya taifa ya England kufuatia kupoteza dhidi ya Argentina, akieleza kuwa kikosi hicho kilicheza vizuri lakini kilifanya makosa yaliyowagharimu kwenye mchezo huo.
Trump alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais wa FIFA, Gianni Infantino, wakati wa shughuli za Kombe la Dunia. Kauli yake ilijikita kwenye namna England ilivyopambana dhidi ya Argentina na namna nahodha Harry Kane alivyotumika katika mchezo huo.
Akizungumzia mchezo huo, Trump alisema England ina wachezaji wenye uwezo na Harry Kane ameendelea kuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi hicho.
"Mna mchezaji mzuri sana huko Uingereza ambaye huwa nacheza naye gofu, Na yeye ni Harry ambaye amekuwa mzuri sana, Nadhani labda walifanya kosa walipomfanya awe mchezaji wa ulinzi," alisema Trump.
Kauli hiyo imeibua mjadala miongoni mwa mashabiki wa soka, hasa kutokana na maoni yake kuhusu nafasi aliyotumika Harry Kane katika baadhi ya vipindi vya mchezo.
Trump alitoa maoni hayo akiwa na Infantino katika hafla ya Kombe la Dunia, huku akisisitiza kuwa anamfahamu Kane kupitia mchezo wa gofu, jambo lililomfanya kueleza mtazamo wake kuhusu mchango wa nahodha huyo ndani ya kikosi cha England.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment