SPAIN WAENDELEZA UBABE MBELE YA UFARANSA , SASA KUREJEREA HISTORIA YA 2010

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya taifa ya Hispania imeibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Ufaransa kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza michuano ya kombe la Dunia na kukata tiketi kucheza fainali na mmoja ya mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Argentina na England.

Huu unakuwa mchezo wa tatu mfululizo kwa ufaransa kupoteza dhidi ya spain baada ya kupoteza 5-4 kwenye mchezo wa Uefa Nationd League na 2-1 kwenye michuano ya Euro, kwa mara nyingine tena wakiwa kwenye ubora mkubwa na kikosi kilicho sheheni nyota wengi bado wameshindwa kutamba na kuondoshwa kwenye michuano.

Ikumbukwe kuwa, hii ni mara ya pili kwa Spain kuingia nusu fainali na kutinga fainali, awali walifanya hivyo mwaka 2010 kwenye mashindano yaliyofanyika Afrika kusini ambapo waliiondosha ujerumani katika nusu fainali kwa ushindi wa 1-0, kisha wakashinda 1-0 dhidi ya Uholanzi kwenye fainali na kutawazwa mabingwa wa michuano hiyo.

Mafanikio waliyoyapata Spain mwaka 2010 huenda yakajirudia tena mwaka 2026, nah ii ni kutokana historia yao ya kutopoteza mchezo wa fainali licha ya kucheza fainali moja walitwaa ubingwa, hii inakuwa fainli yao ya pili na wanauwezo wa kutwaa ubingwa wa pili wamashindano hayo chini ya kizazi cha vijana wao Hodari.

Kwa matokeo hayo funzo linaendelea kutolewa kuwa mpira wa miguu ni mchezo wa dakika tisini na timu iliyojiandaa vizuri ndiyo inayo shinda. Wengi walitarajia ufaransa watacheza fainali ya kombe la Dunia mwaka huu na wengine wakaenda mbali na kuona kuwa wanaweza kutwaa ubingwa, hiyo yote ilichagizwa na ubora wa kikosi chao ambacho kilisheheni nyota hatari wanaocheza vilabu vikubwa barani ulaya lakini Spain wameonyesha kuwa matokeo ya mpira wa miguu yanakuja baada ya dakika tisini.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com





0/Post a Comment/Comments