SIMANZI: NYOTA WA MAMELOD SUNDOWN AFARIKI DUNIA KWA KUJINYONGA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kiungo klabu ya Mamelod Sundown na timu ya taifa ya Afrika Kusini Jayden Adams (25) amefariki Dunia baaa ya kujinyonga wakati akiwa bafuni.

Taarifa zimejiri masaa machache ambapo klabu ya Mamelod ilikuwa ikijiandaa Kwenda Austria kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.

Baada ya kifo hicho kutokea , mlezi na mshauri wa Jayden amevunja ukimya na kueleza kuwa tukio hilo limeicha familia katika mshtuko mkubwa huku wakipitia kipindi kigumu cha kujaribu kukubaliana na hali hiyo huku familia ikiomba kuheshimiwa kwa faragha wakati huu wa maombolezo.

‘Alikuwa na mtazamo Chanya kuhusu kurejea baada ya kombe la Dunia na kuendelea na safari yake, akijua yaliyo kuwa mbele yake .Alikuwa amejiandaa na alifurahia kutumia muda wake nyumbani akiwa Pamoja na familia’

Aidha johnson aliongeza kuwa. ‘hakuna aliye tarajia jambo hili kwa sasa, sina maneno ya kueleza maumivu tuliyonayo lakini tunaomba faragha ya familia iheshimiwe’

Pole kwa wanafamilia wa soka kote ulimwenguni, pole kwa Arika Kusini , poe kwa Mamelod sundown, bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

0767915473,

Lugembetimothy01@gmail.com



0/Post a Comment/Comments